Marekani yawarudisha zaidi ya wahamiaji 50 kutoka Haiti
19 Aprili 2024Msemaji wa wizara ya Usalama wa mambo ya ndani Marekani amesema, sera ya taifa lake haiwaruhusu watu ambao si raia na wasio na msingi wa kisheria kusalia nchini humo.
Afisa wa masuala ya uhamiaji nchini Haiti ameliambia shirika la habari la AFP kwamba jumla ya raia 52 wa Haiti waliwasili katika uwanja wa ndege wa mji wa Cap-Haitien hapo jana Alhamisi.
Soma pia:Mamia ya mashirika yaiomba Marekani kutowarejesha raia wa Haiti wanaokimbia machafuko
Tangu mwishoni mwa mwezi wa Februari, magenge ya uhalifu yenye nguvu yameungana kuanzisha mashambulizi kote nchini nzima, ikiwemo vituo vya polisi, magereza na kusababisha kujiuzulu kwa waziri mkuu Ariel Henry.
Kutokana na mzozo huo unaozidi kuwa mbaya, karibu mashirika 500 ya kutetea haki za binadamu mwezi uliopita yaliandika barua iliyotumwa kwa maafisa wa Marekani akiwemo Rais Joe Biden, wakiomba kusitishwa kurudishwa kwa wahamiaji kutoka Haiti.