1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yawawekea vikwazo jamaa wa Maduro huku hofu ikizidi

12 Desemba 2025

Wizara ya Fedha ya Marekani imewawekea vikwazo ndugu watatu wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro pamoja na makampuni sita yanayosafirisha mafuta kutoka taifa hilo la Amerika ya Kusini.

Marekani Washington D.C. 2025 | Waziri wa Fedha Scott Bessent wakati wa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu vikwazo vya Urusi
Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ikulu ya White House huko Washington, DC, mnamo Oktoba 22, 2025. Picha: Jim Watson/AFP

Taarifa ya Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent imesema waliowekewa vikwazo ni wapwa watatu wa mke wa Maduro, Cilia Flores, akidai kuwa wawili kati yao ni "walanguzi wa dawa za kulevya wanaofanya shughuli zao ndani ya Venezuela."

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Maduro na aliowataja kuwa "washirika wake wa uhalifu" wameingiza dawa nyingi za kulevya Marekani ambazo ni sumu kwa raia.

Washington imechukua hatua hiyo, huku Ikulu ya White House ikisema itaifikisha Marekani meli ya mafuta iliyokamatwa na vikosi vyake hivi karibuni nje kidogo ya pwani ya Venezuela.

Hayo yanajiri wakati kukiwa na hofu ya mzozo unaoendelea kufukuta kati ya nchi hizo mbili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW