Marekani yawawekea vikwazo "waliochangia" mapigano Kongo
25 Agosti 2023Matangazo
Kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara ya fedha ya Marekani, waliowekewa vikwazo ni raia wa Rwanda na Kongo kutoka makundi ya wanamgambo au jeshi wanaoatjwa kuhusika na mapigano na "ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu."
Miongoni mwa hao raia wa Rwanda ni Apollinare Hakizimana na Sebastian Uwibambazi wote wakiwa ni viongozi wa kundi la FDLR la Rwanda.
Soma zaidi:Marais wa jumuiya ya SADC waidhinisha kupelekwa jeshi Kongo
Marekani yazitaka Rwanda, Kongo kuutuliza mvutano
Raia wa Kongo waliowekewa vikwazo ni Bernard Byamungu, ambaye ni kiongozi katika kundi la waasi la M23, na Salomon Tokolonga kutoka kwenye jeshi la Kongo.
Vikwazo hivyo vimepelekea mali zao zilizoko Marekani kufungiwa na ni sharti ziripotiwe.