Marekani yazidisha fedha kugharimia shughuli za kijeshi nchini Irak na Afghanistan
11 Mei 2005Matangazo
Baraza la Senet la Marekani limeidhinisha mabilioni ya dala kugharimia shughuli za wanajeshi wa Marekani nchini Irak na Afghanistan.Jumla ya dala bilioni 82 zimetolewa kwaajili hiyo.Baraza la wawakili limeuidhinisha mpango huo tangu wiki iliyopita.Marekani imetumia jumla ya dala bilioni 300 tangu september 11 mwaka 2001 hadi sasa kugharimia shughuli za wanajeshi wake na mapambano dhidi ya ugaidi.