1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Marekani yazuia ndege za kiraia kwenda nchini Haiti

13 Novemba 2024

Marekani imezuia ndege zote za kiraia kwenda nchini Haiti kwa mwezi mmoja, siku moja baada ya ndege moja ya Marekani kushambuliwa.

Haiti | Uwanja wa ndege wa Port-au-Prince
Uwanja wa kimataifa wa ndege katika mji wa Port-au-Prince ukiwa katika hali ya utulivu katikati ya mapigano ya magenge ya wahalifu nchini HaitiPicha: Odelyn Joseph/AP Photo/picture alliance

Ndege moja ya Marekani ilishambuliwa ilipokuwa ikikaribia kwenye mji mkuu wa Haiti, muda mfupi baada ya Waziri Mkuu mpya kuapishwa.

Hatua hiyo ya Mamlaka ya Anga ya Marekani imefikiwa baada ya ndege ya shirika la Spirit iliyokuwa ikiwasili Port-Au-Prince ikitokea Florida kushambuliwa kwa risasi na kulazimika kubadilisha njia na kwenda Jamhuri ya Dominica.

Hadi jana Jumanne, Haiti ilisalia kama taifa lililotengwa na ulimwengu, wakati uwanja wake mkuu wa ndege ukiwa umefungwa na milio ya risasi ikiendelea kusikika maeneo mbalimbali.

Waziri Mkuu mpya Alix Didier Fils-Aimealiapishwa siku ya Jumatatu akichukua nafasi ya Garry Conille aliyeteuliwa mwezi Mei.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW