Marekani yazuwia utekaji wa meli katika bahari ya Ghuba
27 Novemba 2023Maafisa wa Marekani wameripoti kwamba meli ya mizigo iliyotuma ujumbe wa dharura ikiwa kwenye bahari ya ghuba ya Aden baada ya kutekwa na watu waliokuwa na silaha iko salama, baada ya meli ya kivita ya jeshi la Marekani kuingilia kati.
Katika taarifa yake jeshi la Marekani limesema meli yake ya USS Mason kwa msaada wa meli za washirika wake, iliiwalazimisha washambuliaji kuiachilia Meli hiyo iliyotambuliwa kwa jina la Central Park, iliyokuwa imebeba mzigo wa kemikali.
Washambuliaji watano waliojaribu kukimbia kwa kutumia boti ya mwendo kasi walisalimu amri baada ya kukimbizwa na meli ya kivita ya Marekani.Taarifa ya jeshi la Marekani pia ilisema makombora yalifyetuliwa kutoka maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa Kihouthi nchini Yemen kuelekea meli yao na ile ya mizigo.