1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani,Ulaya zasifu makubaliano Sudan

5 Agosti 2012

Viongozi nchini Marekani na Ulaya wamesifu makubaliano yaliyofikiwa Jumamosi (04.08.2012) kati ya Sudan na Sudan kusini kumaliza mzozo wa mafuta ambao umesababisha matokeo mabaya ya kiuchumi na kutishia kuleta vita.

epa03337058 South Sudanese President Salva Kiir (R) greets US Secretary of State Hillary Clinton (L) in Juba, South Sudan, 03 August 2012. Secretary Clinton arrived in Juba early 03 August as part of her African tour, during which she is visiting Uganda, Kenya, South Sudan, Malawi, Nigeria, Benin and South Africa to promote the United States strategy in regards to Sub-Saharan Africa. EPA/PHILIP DHIL
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton akiwa na rais wa Sudan kusini Salva Kiir mjini JubaPicha: picture-alliance/dpa

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Rodham Clinton , ambaye amefanya ziara Sudan ya kusini kama sehemu ya ziara yake katika bara la Afrika , alitoa sifa hizo kwa nchi zote hizo mbili.

"Tunapongeza ujasiri wa uongozi wa jamhuri ya Sudan ya kusini kwa kuchukua uamuzi huu", amesema. "Muda sasa umefika kufikisha mwisho mkwamo wa mzozo wa mafuta , kwa ajili ya hali bora ya maisha ya watu wa Sudan ya kusini na matarajio yao ya hali bora ya baadaye kutokana na changamoto zinazotokea".

Rais wa Sudan Omar al-BashirPicha: dapd

Ni hali ya kujitoa katika hali mbaya ya uchumi

Amedokeza kuwa makubaliano hayo yanaipa Sudan , nafasi ya kujitoa katika mfadhaiko mkubwa wa kiuchumi ambao unaikumba nchi hiyo. Iwapo Sudan nayo pia itachukua hatua kuelekea amani katika majimbo ya Kordofan ya kusini , Blue Nile na Darfur, na iwapo itaheshimu haki za binadamu za raia zake wote, pia nayo inaweza kuwapa watu wake maisha bora ya baadaye, Clinton amesema.

Ulaya pia yasifu makubaliano

Rais wa Marekani Barack Obama pia amesifu makubaliano hayo. Marekani itaendelea kuunga mkono juhudi za kuendeleza amani ya kudumu kwa watu wa Sudan na Sudan ya kusini, Obama amesema katika taarifa. Nazihimiza pande hizo mbili kutumia kasi iliyopo kutokana na mafanikio haya kutatua masuala yaliyobakia ya mipaka na usalama.

Rais wa Marekani Barack ObamaPicha: Reuters

Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa umoja wa Ulaya , anayehusika na masuala ya mambo ya kigeni Catherine Ashton, amesema kuwa anakaribisha taarifa hizo.

Nazipongeza serikali zote mbili kwa kufikia muafaka ambao umewezesha makubaliano haya na natumai kuwa hali hiyo sasa itaonyeshwa pia katika masuala mengine yaliyobaki, ikiwa ni pamoja na mipaka , jimbo la Abyei na mipango ya usalama, Ashton ameongeza.

Mafanikio hayo yalitangazwa mapema Jumamosi, wakati mpatanishi mkuu Thabo Mbeki alipowaambia waandishi habari kuwa "mafuta sasa yataanza kutiririka tena", katika taarifa aliyoitoa katika mkutano wa baraza la usalama na amani la umoja wa Afrika, katika mji mkuu wa Ethiopia , Addis Ababa.

Rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo MbekiPicha: AP

Baraza hilo lilikutana kujadili jinsi ya kutatua mzozo huo kati ya nchi hizo mbili baada ya kushindwa kufikia makubaliano juu ya usalama na mafuta , kabla ya kumalizika muda wa mwisho uliowekwa na baraza la usalama la umoja wa mataifa wa August 2.

Januari mwaka jana , Sudan ya kusini ilifunga uzalishaji wa mafuta baada ya Sudan kutaifisha mafuta ghafi yenye thamani ya dola milioni 815 ya Sudan kusini, ambayo imedai ni malipo ya ushuru ambao haujalipwa.

Mei mwaka huu, umoja wa mataifa uliamuru kwa kitisho cha kuweka vikwazo kuwa pande hizo mbili zisitishe uhasama, ziondoe majeshi yao kutoka katika jimbo linalogombaniwa la Abyei na kukubaliana malipo ya ushuru wa mafuta katika muda wa miezi mitatu.

Mazungumzo mengine yamesitishwa hadi baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan baadaye mwezi huu.

Mwandishi : Sekione Kitojo / dpae

Mhariri: Mtullya Abdu

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW