1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUbelgiji

Mark Rutte kuongoza mkutano wa mawaziri wa Ulinzi wa NATO

17 Oktoba 2024

Mawaziri wa ulinzi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO wako mjini Brussels kwa mkutano wa siku mbili unaoanza Alhamisi.

Brüssel | Katibu Mkuu wa NATO, Mark Rutte
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Mark RuttePicha: SIMON WOHLFAHRT/AFP

Mkutano huo utaangazia vita vya Ukraine, mustakabali wa ulinzi wa jumuiya hiyo na kiwanda cha kutengeneza vifaa vya kijeshi.

Katibu Mkuu wa NATO, Mark Rutte atauongoza mkutano huo kwa mara ya kwanza tangu achukue wadhfa huo. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na waziri wake wa ulinzi, Rustem Umerov wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.

Zelensky ametaka apewe mwaliko wa mara moja wa kujiunga na NATO na amerudia wito wake wa kutaka vikwazo vya kushambulia ndani ya Urusi kwa makombora ya masafa marefu viondolewe. China, Urusi, Korea Kaskazini na Iran pia zitakuwa kwenye ajenda ya mkutano huo.