1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron ataka kusitisha kuingia nchini Ufaransa kwa ma imamu

Saleh Mwanamilongo
19 Februari 2020

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kusitishwa kuingia nchini Ufaransa kwa ma imamu kutoka nje kwa ajili ya kufundisha uislamu nchini humo.

Paris Präsident Macron
Picha: AFP/G. Fuentes

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kusitishwa kwa kuajiriwa kwa maimamu kutoka nje kwa ajili ya kufundisha uislamu nchini Ufaransa. Hayo ameyasema wakati wa ziara yake mashariki mwa nchi ambako kuliripotiwa visa vya hisia za kujitenga kutokana na misingi ya kidini. Wakati huohuo amelezea kwamba hatua zitachulukiwa ili kupambana na kubaguliwa kwa Waislamau nchini Ufaransa. 
Rais Emmanuel Macron amesema Jumanne kwamba anataka kuchukuwa hatua kali katika kupambana na mahubiri ya itikadi kali za kidini na kubaguliwa kwa Waislamu nchini mwake.
Rais huyo wa Ufaransa aliita msimamo mkali wa kujitenga  kuwa ni adui ambaye hauambatani na uhuru,usawa na umoja wa taifa. Aliyasema hayo wakati wa ziara yake kwenye mji wa Mulhouse ,masharaki mwa ufaransa.
Akizungumza mjini Mulhouse, Macron alisema, ''Leo tuna ma imamu 300 ambao wanaletwa Ufaransa kila mwaka, na  waliofika mwaka 2020 watakuwa wa mwisho kwa idadi hiyo kuwasili hapa.''
 ''Tutaanza kupunguza idadi yao, hadi hapo hatutapokea ma imamu wapya. Hawa ambao tayari wamewasili watabaki hapa hadi mwisho wa kipindi chao cha miaka mitatu'' Aliongeza Macron.

Picha: picture-alliance/AP/F. Mori


Kiongozi huyo wa Ufaransa amewaonya wanaovunja sheria, akisema ''Hatuwezi kutekeleza sheria za Uturuki kwenye ardhi ya Ufaransa'' alisema Macron.
Aliongeza akisema kwamba sheria za kidini haziwezi kuwa juu ya sheria za kitaifa.
Rais wa Ufaransa amependekeza kuongeza maimamu waliopewa kupewa mafunzo nchini Ufaransa.
 ''Tunataka kupunguza hatua kwa hatua idadi ya maimamu kutoka nje na hata wale wanaokuja kila mwaka wakati wa mwezi wa ramadhan ambao ni 300.''
 Hatua kali pia zitachukuliwa ili kuchunguza misaada kutoka nje kwa ajili ya maeneo ya ibada, kuhakikisha kwamba fedha zinazotolewa ni halali.

Rais Macron aliyasema hayo mbele ya viongozi na raia wa mji wa Mulhouse, ambako kunaripotiwa visa vingi vya kutovumiliana kidini. Amewambia raia wa mkoa wa Bourtzwiller kwamba vita dhidi ya misimamo ya kujitenga haiwalengi tu waislamu.
Ziara  hiyo ya Rais Emmanuel Macron mashariki mwa nchi yake ni hatua ya mwanzo itakayoendelea hadi baada ya uchaguzi mdogo wa mwezi ujao, ambapo anazinadi sera zake za kupambana na kuweko mitazamo mikali ya kidini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW