1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghana iliweka marufuku ya kuzwa pilipili na mabiringanya

19 Juni 2019

Wakulima wa mboga nchini Ghana wana matumaini kwamba marufuku ya kupeleka bidhaa zao za shambani Ulaya yataondolewa baada ya maafisa wa kilimo wa Ghana kuanza kuyakagua mashamba yao yanayodaiwa kuwa na wadudu hatari

DW Eco Africa - Ghana Kakao
Picha: DW

Mwezi wa Mei serikali ya Ghana iliweka marufuku ya kusafirishwa kwa pilipili na mabiringanya kwenda Ulaya kwa hofu  kwamba yako na wadudu na viini hatari vinavyoweza kusababisha maradhi. Serikali ya Ghana imechukua uamuzi huo wakichelea Ulaya kuwawekea marufuku mengine yatakayodumu muda mrefu kama ilivyoweza kufanya miaka iliyopita.

Marufuku ya Ulaya iliondolewa hivi karibuni baada ya kudumu kwa zaidi ya miaka miatatu. Waziri wa kilimo wa Ghana Owusu Afriyie Akoto amesema kwa sasa wanafanya kila njia kuhakikisha wakulima wanapata dawa za kuhakikisha mazao yao hayashwikwi na wadudu.

"Tumechukua tahadhari wenyewe. tunajaribu kuzuilia jumuiya ya kimataifa kutuchukulia hatua ya kutuwekea vikwazo kama ilivyotufanyiwa mwaka 2015. Kwa hivyo kujikakugua wenyewe ni ishara nzuri kutoka kwa wizara ya chakula na kilimo kwamba tuko tayari kulinda thamani ya vyakula vyetu, vyakula tunavyouzwa mataifa ya nje na kila kitu," alisema Akoto.

Mmoja wa wakulima wadogo wadogo nchini Ghana akiwa na jembe lake beganiPicha: DW

Mkulima wa zaidi ya miaka kumi, Mashariki mwa Ghana, Issah Mohammed alisema kutokana na ughali wa bei za dawa za wadudu wakulima wengi wanashindwa kupuliza dawa katika mashamba yao, anaeleza kwamba ukulima umekuwa mgumu na wakulima wengi hawana pesa kwa hivyo serikali inahitajika kupunguza gharama ya dawa hizo. Issa anaongeza kwamba kwa sababu ya kutoweza kununua dawa, mazao mengi ya wakulima hayatakuwa na hali nzuri kwa ajili ya kuuzwa Ulaya.

Wafanyabiashara wakosoa marufuku hiyo

Muungano wa Ghana wa wauzaji maboga katika mataifa ya nje kupitia kiongozi wake Samuel Nii Taki ulieleza kutofurahishwa na marufuku hiyo ambayo haikulazimu kutokana na hali ngumu za wakulima.

"Kinachotuudhi ni kwamba hatukuhuishwa, Pili ni kwamba miaka mitatu iliyopita tulikubaliana kwamba kunapotokea tatizo katika shamba fulani, mkulima asimamishwe kulima kisha kuelekezwa kurekebisha kabla ya kuruhusiwa tena kutoa mazao kwa ajili ya biashara ila hilo halikufanyika. Kulipowekwa marufku mara ya kwanza wakulima waliingia hasara kwa kupoteza pesa nyingi na kupoteza biashara nyingi na hata ilipoondolewa marufuku hiyo wakulima hawakuwa na nia sya kuendelea kufanya kilimo," alisema Taki.

Ni muda tangu Ghana kuweka marufuku hiyo ya pilipili na mabiringanya. Bidhaa hizo sasa zinahofiwa kwamba zitalazimika kuuzwa katika masoko ya Ghana, japo Samuel anasema kwamba vyakula hivyo vinatumiwa sana na jamii za Asia kwa hivyo haziwezi kupata soko Ghana na kilichopo ni kwamba wakulima na wasafirishaji ndio wanaoingia hasara kwa sababu hawana mahali pa kupeleka mazao hayo.

Kwa sasa maafisa wa kilimo cha matunda na maboga nchini Ghana wanaendelea na kuyafanyia ukaguzi mashamba mbalimbali na wakulima ambao mashamba yao yatakapatikana salama hayana wadudu ndio watakoruhusiwa kuendelea kulima na kuuza Ulaya.

(DW)

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW