SiasaMarekani
Maseneta wa Marekani wachapisha rasimu ya mpango wa usalama
5 Februari 2024Matangazo
Mpango huo unaofahamika zaidi kama "msaada wa ziada wa usalama" unajumuisha jumla ya dola bilioni 118.3, zikiwemo dola bilioni 60 za kuisaidia Ukraine kukabiliana na uvamizi wa Urusi, dola bilioni 14.1 kwa ajili ya Israel na dola bilioni 20.2 za kuimarisha usalama kwenye mipaka ya Marekani.
Soma pia: Zelensky kuwahutubia maseneta wa Marekani kufuatia msaada uliozuiliwa
Matarajio ya rasimu hiyo yenye kurasa 370 kuwa sheria bado ni hafifu kutokana na mivutano ya kisiasa. Rais Joe Biden amewatolea wito wabunge wa Republican kuunga mkono rasimu hiyo inayotarajiwa kujadiliwa Bungeni wiki hii.