1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashabiki wa soka Ujerumani waonywa

Deo Kaji Makomba
12 Mei 2020

Mamlaka nchini Ujerumani imewaonya mashabiki wa soka nchini hapa kwamba mechi huenda zikafutwa endapo mashabiki watajikusanya kwa wingi nje ya uwanja kufuatilia mechi hizo za Bundesliga

Deutschland Freiburg | Fussball Bundesliga | SC Freiburg vs.1. FSV Mainz 05
Picha: picture-alliance/dpa/G. Gruendl

Soka la Ujerumani ambalo ni miongoni mwa ligi kubwa barani Ulaya litawasha moto wake kwa kuanza tena ikiwa ni miezi miwili kupita baada ya kusitishwa kwa muda kutokana na marufuku iliyowekwa ya watu kutokusanyika ili kuiepusha uwezekano wa maambukizi mapya ya virusi vya Corona kuenea, lakini mkakati wake umegubikwa na hatari.

Katika nchi yenye wazimu wa mpira wa miguu ambayo inajivunia wastani wa mahudhurio ulimwenguni, je! Wafuasi waliofukuzwa kwenye uwanja wataweza kukaa mbali? Hilo ndio swali linalogonga vichwa vya wengi hapa Ujerumani.

Katika jimbo la Saxony lililopo Ujerumani Mashariki ambapo wenyeji RB Leipzig wanaoshikilia nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo, watawakaribisha  Freiburg Jumamosi alasiri, huku Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Roland Woeller akitoa tishio la wazi kwa mashabiki lialia wa soka.

"Mashabiki sio lazima washuhudie  mechi nyuma ya milango iliyofungwa kama kisingizio cha kukusanyika mbele ya uwanja au mahali pengine," alisema Woeller na kuongeza kuwa hii inaweza kusababisha mechi kusimamishwa.

Mamia kadhaa ya mashabiki wa soka walikusanyika katika mechi ya  Moenchengladbach wakati wenyeji wakiishindilia Cologne 2-1 mnamo tarehe 11 mwezi Machi, mchezo wa kwanza wa ligi ya Ujerumani uliochezwa bila ya kuwa na mashabiki nyuma ya milango iliyofungwa, siku chache kabla ya ligi hiyo kusimamishwa.

Klabu ya soka ya Eintracht Frankfurt imetoa wito kwa mashabiki wao kabla ya kuanza msimu wao dhidi ya 'Gladbach Jumamosi. "Tumeongea mengi na Mashabiki wetu na tukasema: 'sikilizeni, msije kwenye uwanja'," mkurugenzi wa michezo wa Frankfurt Fredi Bobic aliiambia ESPN.

Katika sheria za ligi ya soka ya Ujerumani zilizowekwa ili kuanza tena msimu, upande wa nyumbani unawajibika kwa kuhakikisha mashabiki hawajaribu kukaribia uwanja na kwamba waiunge mkono timu yao wakiwa mbali na uwanja.

Baada ya wiki kadhaa za mipango ya kina na upimaji wa wachezaji na wafanyakazi, itakuwa ndoto ya Bundesliga ikiwa mashabiki wangeondoa jaribio dhaifu la urejeshwaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya ligi ya Bundesliga ataka mashabiki kuwa watulivu

Mashabiki wa soka wakionyesha mabango uwanjaniPicha: Getty Images/AFP/S. Schuermann

Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya ligi ya Bundesliga, Christian Seifert, amesema kuwa hatarajii mashabiki kucheza mikononi mwa wakosoaji ambao wanaogopa watafanya nje ya uwanja licha ya matukio makubwa ya umma kufungiwa nchini Ujerumani kutokana na mripuko wa virusi vya Corona.

Seifert alishtumu wakosoaji wanaotabiri kwamba wapenzi wa mpira wa miguu watashindwa kuheshimu maombi hayo ya kujizuia kufanya.

"Siamini kuwa eneo la shabiki na mashirika ya shabiki watawafanya wakosoaji wao kupata cha kusema," alisema bosi huyo wa  undealiga na kuongeza kuwa mazungumzo yote ambayo alikuwa ameuafanya juu ya suala hilo "haitoi dalili yoyote" kwamba wafuasi watakusanyika.

Kituo cha matangazo ya runinga cha Sky kimekubali kuonyesha mechi zingine za Jumamosi kwenye chanaeli ya bure, ikitoa hofu kwamba mashabiki watakusanyika kwenye baa au sehemu za umma ambazo zina usajili kwa huduma ya utazamaji wa malipo.

Ingawa, Seifert anasema wakati wanachukua kila hatua stahiki kuwakatisha tamaa mashabiki kukusanyika, lakini jukumu la DFL linaisha kwa hatua fulani.

Kitovu cha kurudi kwa hatua Macho na masikio ya wapenzi wa soka nchini Ujerumani na barani Ulaya jumamosi hii yataelekezwa kwenye uwa ja wa  Signal Iduna ParkJumamosi hii ambapo wenyeji Borussia Dortmund watawakaribisha Schalke ikiwa ni mechi Derby ambayo kawaida inaweza kuteka umati wa watu 82,000 katika uwanja uwanja huo endapo mashabiki wakiruhusiwa kuingia uwanjani.

Badala yake, itakuwa mara ya kwanza kwa ratiba hii mechi kucheza nyuma ya milango iliyofungwa bila maishabiki uwanjani tangu ilipoanza mnamo 1925.

Viwanja vikubwa vya Ujerumani kwa mfano Allianz Arena unaotumiwa na klabu ya Bayern Munich wenye uwezo wa kubeba watazamani 75,000 utabaki tupu kwa mustakabali unaoweza kutarajiwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW