1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashabiki wapinga kelele bandia viwanjani

Deo Kaji Makomba
17 Juni 2020

Vikundi vya mashabiki wa soka kutoka sehemu mbalimbali barani Ulaya vimekosoa hatua ya kurushwa mubashara kwa mechi za ligi mbalimbali barani humo bila mashabiki huku kukitumiwa kelele za mashabiki bandia

Deutschland Mönchengladbach | Sport & Coronavirus | Fußball, Papp-Fans
Picha za mashabiki bandia wa sokaPicha: Reuters/T. Schmuelgen

Vikundi vya mashabiki wa soka kutoka sehemu mbalimbali barani Ulaya vimekosoa hatua ya kurushwa mubashara kwa mechi za ligi mbalimbali barani humo bila mashabiki huku kukitumiwa kelele na picha bandia za mashabiki na kuelezea kuwa kitendo hicho ni kama kejeli kwa wapenzi na mashabiki wa soka.

Mashabiki hao wa soka walisema kuwa kurejea kwa hivi karibuni kwa mechi za soka za ligi mbalimbali, bila mashabiki baada ya kusimamishwa kufuatia mripuko wa janga la virusi vya Corona, ilionyesha kwamba mashabiki wa soka ni uti wa mgongo wa mchezo na mchango wao unapaswa kuthaminiwa katika ligi na klabu.

"Tunao wasiwasi mkubwa kuhusu majaribio ya vyombo vya habari ikiwemo luninga kuiga hali ya kipekee inayotokana na mashabiki," ilieleza taarifa ya kikundi cha mashabiki wa soka barani ulaya, ambayo pia ilisainiwa na vikundi 26 vya mashabiki kutoka katika nchi za Ulaya.

"Kuongezeka kwa teknolojia, ujumbe uliorekodiwa na aina nyingine za kelele bandia inawakilisha kejeli kwa mashabiki wa soka," ilisema taarifa hiyo. "Kutokuwepo kwa mashabiki uwanjani hakuwezi kufidiwa kwa komputa inayolenga kufurahisha watazamaji wa soka kupitia luninga."

Baadhi ya makampuni ya utangazaji kama vile Sky la Ujerumani limewapa watazamaji chaguo la kutizama michezo na kelele za umati bandia, wakati katika nchi nyingine kama vile Hungary ambapo kelele bandia za mashabiki zimeingizwa kwenye uwanja wenyewe.

Reuters

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW