Mashambulio ya Israel na Iran yaendelea kutikisa
9 Machi 2026
Israel imeendelea na operesheni za kijeshi dhidi ya maeneo kadhaa nchini Iran na Lebanon leo Jumatatu.
Jeshi la nchi hiyo limefahamisha kupitia taarifa kwenye mtandao wa Telegram, kwamba wimbi la mashambulizi ya anga yamefanywa dhidi ya miundo mbinu ya utawala wa Iran, na kundi lenye mafungamano na utawala huo la Hezbollah mjini Beirut.
Iran yaingia enzi mpya ya uongozi wa Mojtaba huku vita ikienea
Iran pia imefanya mashambulio mengine zaidi dhidi ya Israel na mataifa ya Ghuba leo Jumatatu saa kadhaa zikiwa zimepita baada ya kumtangaza Mojtaba Khamenei kuwa kiongozi wa juu anayerithi nafasi ya babake aliyeuliwa na Marekani, Ayatollah Ali Khamenei.
Kufuatia mashambulio hayo yaliyolenga pia kinu cha mafuta cha Saudi Arabia cha Shaybah, Riyadh imeionya Iran kwa maneno makali, ikisema nchi hiyo itashindwa vibaya ikiwa itaendelea kuyashambulia mataifa ya kiarabu.