1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MASHAMBULIO YA ISRAEL YALAANIWA

24 Desemba 2003
NEW YORK: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ameyalaani mashambulio ya Israel katika kambi ya Rafah ya wakimbizi wa Kipalestina.Annan amesema katika mashambulio hayo kwenye Ukanda wa Gaza,vikosi vya Israel vimetumia nguvu zilizopindukia.Israel iliokalia eneo hilo ina wajibu wa kuwalinda wakaazi alisisitiza Kofi Annan.Kwa wakati huo huo alitoa muito kwa pande zinazozozana kurejea katika majadiliano ya amani. Wapalestina 8 wamauliwa na zaidi ya 40 wamejeruhiwa katika mashambulio ya Rafah.Israel imesema lengo la opresheni hiyo ni kusaka njia za chini kwa chini zinazotumiwa kusafirisha silaha za magendo.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW