Mashambulio ya kigaidi yaua 91 nchini Norway
23 Julai 2011Mtu aliejifanya kuwa polisi aliingia katika kisiwa hicho na kufyatua risasi.Polisi wamemkamata mtu mmoja mwenye umri wa miaka 32 kuhusiana na mashambulio hayo. Mawasiliano ya mtandao wa Internet ya mtuhumiwa huyo, yameashiria kuwa yeye ni mtu mwenye itikadi kali za mrengo wa kulia. Hata hivyo, hakuna ishara zinazoonyesha kuwa mtu huyo anahusiana na magaidi wa kimataifa.
Wakati huo huo, serikali za nchi mbalimbali duniani zimelaani mashambulio hayo ya kigaidi. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa ameshtushwa na mashambulio hayo na kwamba serikali yake na watu wa Ujerumani watasimama pamoja na watu wa Norway.
Umoja wa Ulaya pia umesema umeshtushwa na kile kilichoitwa mashambulio ya kutia uchungu yaliyofanywa katika nchi inayosifika kwa juhudi zake za kuleta amani duniani.
Rais Barack Obama ametoa rambi rambi kwa watu wa Norway. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, William Hague pia ametoa rambi rambi kwa wahanga na familia za watu waliothirika na mashambulio na amelaani aina zote za ugaidi.