1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Mashambulio ya Pakistan yaua watu kadhaa Afghanistan

18 Machi 2024

Serikali ya Afghanistan imesema watu wanane nchini humo wameuawa kutokana na mashambulio yaliyofanywa na Pakistan.

Mvutano kwenye mpaka kati ya Pakistan na Afghanistan umeongezeka tangu serikali ya Taliban ilpoingia madarakani mwaka 2021.
Mvutano kwenye mpaka kati ya Pakistan na Afghanistan umeongezeka tangu serikali ya Taliban ilpoingia madarakani mwaka 2021.Picha: Inter-Services Public Relations/REUTERS

Afghanistan imeeleza kuwa ndege za Pakistan zilizishambulia nyumba za raia, siku mbili baada ya waasi kufanya shambulio la kujitoa mhanga na kuwaua wanajeshi saba wa Pakistan. 

Msemaji wa utawala wa Taliban nchini Afghanistan Zabihullah Mujahid amesema, waliouawa walikuwa watoto watatu na kina mama watano kwenye majimbo ya mpakani.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji huyo, ndege za jeshi la Pakistan ziliyashambulia majimbo ya Khost na Paktika karibu na mpaka wa Pakistan leo alfajiri.

Mvutano kwenye mpaka kati ya Pakistan na Afghanistan umeongezeka tangu serikali ya Taliban ilpoingia madarakani mwaka 2021, huku Pakistan ikidai kuwa makundi ya wanamgambo yanafanya mashambulizi ya mara kwa mara kutoka nchi Jirani ya Afghanisatan.