1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel yaishambulia vikali Gaza

27 Machi 2024

Israel imefanya mashambulizi makali katika eneo la Kusini mwa Ukanda wa Gaza licha ya shinikizo za kimataifa la kusitishwa mara moja kwa mapigano katika eneo hilo la Palestina linalokabiliwa na tishio la njaa.

Uharibifu baada ya mashambulizi ya Israel huko Gaza
Mtazamo kutoka eneo lililoharibiwa baada ya shambulio la Israeli huko Deir al-Balah, Gaza mnamo Machi 20, 2024. Israel inaendeleza mashambulizi makubwa katika eneo la Ukanda wa GazaPicha: Ashraf Amra/Anadolu/picture alliance

Wizara ya afya inayosimamiwa na kundi la wanamgambo wa Hamas katika eneo hilo, imesema mapema leo kwamba watu 66 wameuawa katika shambulizi hilo ikiwa ni pamoja na watu wengine watatu waliouawa katika shambulizi la Israel katika eneo la Rafah.

Mapigano hayo yameendelea siku mbili baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio lake la kwanza la kutaka kusitishwa mara moja kwa mapigano na kutaka kuachiliwa kwa takriban mateka 130 ambao Israel inasema wamesalia Gaza, wakiwemo mateka 34 wanaodhaniwa kuwa wamekufa.

Wizara hiyo pia imesema, vikosi vya Israel vimezingira hospitali mbili katika eneo la Khan Yunis ambapo watu 12 wanaowajumuisha watoto waliuawa katika shambulizi la vikosi hivyo dhidi ya kambi moja ya wakimbizi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW