Mashambulizi ya Urusi yaua raia wawili wa Ukraine
5 Oktoba 2023Andriy Yermak, Mkuu wa ofisi ya Rais Zelensky amesema kwenye mtandao wake wa Telegram kwamba watu wawili wamekufa, akiwemo mfanyakazi wa idara ya umma, kufuatia mashambulizi ya anga ya Urusi kwenye mji wa kusini mwa Ukraine wa Kherson.
Awali, serikali ya Ukraine ilisema kwamba mifumo yake ya ulinzi wa anga iliharibu ndege zisizo na rubabi 24 miongoni mwa 29 zilizorushwa na vikosi vya Urusi usiku wa kuamkia leo. Ndege hizo zisizo na rubani za aina ya Shahed-131/136 zililenga maeneo ya Odesa, Mykolaiv na Kirovograd, yaliko katikati na kusini mwa Ukraine.
Maafisa wa kijeshi wanaohusika na kusini mwa nchi hiyo walisema Urusi inaendelea na juhudi zake za kuharibu bandari na miundombinu mingine kusini mwa Ukraine. Taarifa ya jeshi la Ukraine iliongeza kusema kuwa kituo cha miundombinu katika mkoa wa Kirovograd kilishambuliwa na makombora ya urusi, bila kutoa maelezo zaidi.
Kwa upande wake Urusi imeishutumu Ukraine kwa Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye miji miwili midogo ya vidogo magharibi. Gavana wa jimbo laUrusi la Kursk, Roman Starovoyt, amesema mashambulizi hayo yalisabbabisha kutakika kwa umeme katika miji 67.
''Tunafanya kila tuwezalo''
Wakati huohuo rais Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky yoko mjini Granada, Uhispania ili kuhakikisha usalama na utulivu wa pamoja wa bara la Ulaya. Amesema Ukraine ina mapendekezo makubwa ikiwemo kuzingatia usalama wa usafirishaji chakula kupitia Bahari Nyeusi. Rais Zelensky amesema anatarajia pia msaada zaidi wa silaha kutoka kwa washirika wa Ukraine.
"Tunafanya kila tuwezalo kuipatia Ukraine mifumo zaidi ya ulinzi wa anga kabla ya msimu wa baridi. Na sasa, tunatarajia maamuzi fulani kutoka kwa washirika wetu. Lakini kazi yote katika mikoa ambayo inahusiana na ulinzi wa raia na wa vifaa muhimu na ujenzi wa haraka lazima ikamilike haraka iwezekanavyo wakati wa msimu wa baridi.'', alisema Zelenksy.
Maafisa kutoka Shirika la Fedha Ulimwenguni IMF wanasema wanatarajia Marekani itaendelea kutekeleza jukumu lake kuu katika kukusanya msaada wa kimataifa ambao umesaidia uchumi wa Ukraine katika kipindi hiki cha uvamizi wa Urusi.
Huku hayo ya kijiri Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu na Mkuu wa majeshi ya nchi hiyo Jenerali Valery Gerasimov, walifanya mkutano na makamanda wa jeshi wanaopigana nchini Ukraine. Hata hivyo, kufahamika mara moja ni wapi mkutano huo ulifanyika. Wizara ya ulinzi ya Urusi ilitangaza picha za waziri Shoigu akihutubia vikosi vya wanajeshi pamoja na wapiganaji wa kujitolea kwenye kambi wanakopewa mafunzo.
Vyanzo: AFP, Reuters, DPA