1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIraq

Mashambulizi ya anga ya Iraq yamuua mmoja wa viongozi wa IS

18 Oktoba 2024

Jeshi la Marekani linadai kuwa mashambulizi ya anga ya Iraq yamemuua kiongozi mkuu wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, ISIS, na wanamgambo wengine watatu.

Mashambulizi ya anga ya Iraq yamuua mmoja wa viongozi wakuu wa ISIS
Mashambulizi ya anga ya Iraq yamuua mmoja wa viongozi wakuu wa ISISPicha: piemags/IAMGO

Kwa mujibu wa Marekani, mashambulizi hayo yaliwezeshwa na muungano wa kimataifa wa kijasusi unaopambana na makundi ya kigaidi.

Taarifa hiyo iliyochopishwa katika mtandao wa kijami imesema vikosi vya usalama vya Iraq (ISF) vilifanya mashambulizi ya anga kaskazini mashariki mwa Iraq mnamo Oktoba 14 na kuwaua wanachama wanne wa kundi la ISIS,akiwemo kiongozi wao anayejulikana kama Shahadhah Allawi Salih al-Bajjari, anayejulikana pia kwa jina la Abu Issa.

Mashambulizi hayo yanakuja baada ya vikosi vya Marekani na Iraq kufanya operesheni ya pamoja mwishoni mwa mwezi Agosti ambayo kamandi ya Marekani ilisema iliwaua wanachama 14 wa kundi la ISIS, miongoni mwao viongozi wanne.

Marekani ina takribani wanajeshi 2,500 nchini Iraq na 900 nchini Syria kama sehemu ya muungano huo, ambao Washington na Baghdad zilitangaza mwezi uliopita kuwa utamaliza muda wake wa muongo mmoja nchini Iraq ndani ya mwaka mmoja.