1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mashambulizi ya anga ya Israel yawaua watu 9 huko Gaza

4 Februari 2026

Shirika la ulinzi wa raia la Gaza limesema mashambulizi ya anga ya Israel yamewaua watu tisa katika eneo la Wapalestina, ikiwemo watoto watatu.

Misri Rafah 2026 | Magari ya wagonjwa upande wa Misri yakisubiri kwenye kivuko cha mpaka cha Rafah ili kifunguliwe
Kivuko cha Rafah kilichofunguliwa tena hivi karibuni na IsraelPicha: Ahmed Sayed/Anadolu/picture alliance

Shirika la ulinzi wa raia la Gaza limesema mashambulizi ya anga ya Israel yamewaua watu tisa katika eneo la Wapalestina, ikiwemo watoto watatu huku jeshi la Israel likisema kwamba lilishambulia baada ya mashambulizi ya risasi yaliyowalenga wanajeshi wake na kumjeruhi afisa mmoja.

Mashambulizi hayo yametokea siku chache baada ya Israel kukifungua tena kivuko cha Rafah kati ya Gaza na Misri, ambacho ni kivuko pekee kinachowasaidia watu wa Gaza wasiopitia Israel.

Licha ya makubaliano yaliyoratibiwa na Marekani kuingia awamu ya pili mwezi uliopita, machafuko yameendelea katika Ukanda wa Gaza, huku Israel na Hamas zikitupiana lawama kwa kukiuka makubaliano hayo.

Wakati huo huo, mjumbe maalum wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati Steve Witkoff alifanya mazungumzo hapo jana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

  

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW