1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAsia

Wanafunzi 19 wauwawa kwa mashambulizi ya anga Myanmar

13 Septemba 2025

Wanamgambo wa jamii ya walio wachache nchini Myanmar wamesema takriban wanafunzi 19 wameuawa katika mashambulizi ya anga wanayodai yamefanywa na wanajeshi, magharibi mwa jimbo lenye mzozo la Rhakhine.

Myanmar 12.09.2025
Muonekano wa sehemu ya eneo kwenye moja ya shule mbili zinazodaiwa kushambuliwa na jeshi la Myanmar Picha: AP Photo/picture alliance

Wanamgambo hao wa Arakan kupitia chaneli yao ya telegram leo Jumamosi wamebainisha kwamba mashambulizi yalizilenga shule mbili binafsi za sekondari. Wanafunzi waliouawa wana umri kati ya miaka 15 na 21 wakati wanafunzi wengine 22 wamejeruhiwa. Jeshi la Myanmar hajatoa kauli yoyote kuhusu mashambulizi ya leo.

Mzozo wa Rakhine ni sehemu ya machafuko yaliyojaa umwagaji damu yanayoitesa Myanmar, tangu jeshi lililpoipindua serikali ya kiraia ya  Aung San Suu Kyi mwaka 2021. Tangu hapo, watawala wa kijeshi wanakabiliwa na upinzani kutoka kwa makundi yanayowapinga.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW