1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Mashambulizi ya anga yamewaua 11 Syria

25 Juni 2023

Watu kumi na mmoja wameuwawa leo Jumapili, baada ya Urusi kufanya mashambulizi ya anga kaskazini magharibi mwa Syria.

Syrien, Idlib | Russischer Luftangriff
Picha: Ä°zzeddin Kasim/AA/picture alliance

Mkuu wa shirika la uangalizi wa haki za binadamu la Syria Rami Abdel Rahman amesema miongoni mwa waliouwawa ni raia saba.

Kwa mujibu wa shirika hilo, mashambulizi hayo ya anga yalilenga soko la matunda na mboga ambalo wakulima hulitumia kama chanzo cha mapao yao.

Soma pia: Watu wawili wauawa katika shambulizi la angani Syria

Taarifa iliyotolewa na Ahmed Yezidi wa vikosi vya ulinzi wa raia katika mji wa Jisr al Shugur unaodhibitiwa na waasi, takribani watu 30 wamejeruhiwa katika tukio hilo na huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

Mashambulizi hayo yanatajwa kuwa ni ya kulipiza kisasi baada ya ndege zisizo na rubani kufanya mashambulizi yanayodaiwa kuwa yalifanywa na vikosi vya  waasi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW