1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mashambulizi ya angani yaendelea kuutikisa mji mkuu wa Sudan

25 Juni 2023

Milio ya risasi na mashambulizi ya angani kwa mara nyengine yameutikisa mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Sudan | Sicherheitskräfte
Picha: Ashraf Shazly/AFP/Getty Images

Umoja wa Mataifa ukihimiza kusitisha "mauaji ya kiholela" ambayo yameacha miili ya watu waliouwawa ikoza katika jimbo la Darfur.

Wakizungumza na shirika la habari la AFP baadhi ya wakaazi wamesema wilaya zote za Khartoum hazina tena maji ya bomba, na wale waliosalia katika jiji hilo hawana umeme kabisa tangu Alhamisi.

Soma pia: Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa latoa wito wa kusimamisha mapigano nchini Sudan

Kulingana na shirika linalojishughlisha na ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa katika maeneo ya mizozo la ACLED,  Vita vya kugombea madaraka kati ya mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani, kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Daglo, vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000.

Soma pia: Wafadhili wachangia dola bilioni 1.5 kuisaidia Sudan

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa takriban watu milioni 1.5 wameukimbia mji mkuu Khartoum tangu kuzuka kwa ghasia nchini humo katikati ya mwezi wa Aprili.

Hadi sasa, hakuna upande unaoonekana kuwa tayari kusitisha mapigano na hivyo kuzidisha hatari ya mzozo wa muda mrefu wa kikanda.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW