1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya droni Kongo yatishia juhudi za amani

14 Machi 2026

Serikali ya Kongo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameshtumiana kwa kukiuka masharti ya makubaliano ya kusitisha mapigano yenye lengo la kumaliza mzozo wa miongo kadhaa na kuleta amani ya kudumu.

Kongo Goma 2025 | M23
Wapiganaji wa M23 wawasindikiza wanajeshi wa serikali waliojisalimisha kuelekea eneo ambalo halikutambulishwa mjini Goma mnamo Januari 30, 2025Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Msemaji wa M23 Lawrence Kanyuka ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba kundi hilo litaendelea kuonyesha nia thabiti kwa juhudi za amani ikiwa jeshi la Kongo litaepuka kushambulia maeneo yao na kuwauwa viongozi wao, wanajeshi na raia wasiokuwa na hatia.

Kwa upande wake, msemaji wa serikali ya Kongo Patrick Muyaya amesema serikali inachunguza shambulizi la wiki hiii lililomuuwa mfanyakazi wa shirika la misaada raia wa Ufaransa, lakini hakufafanua zaidi kuhusu mashambulizi mengine ya droni.

Muyaya ameilaumu M23 kwa kukiuka makubaliano ya kusitishaji mapigano, lakini akasema kuwa upande wa serikali ungependa kusisitiza tena kujitolea kwao kuheshimu makubaliano hayo ya kusitisha mapigano pamoja na makubaliano mengine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW