Migogoro
Mashambulizi ya Urusi yawauwa watu saba Ukraine
8 Machi 2026
Matangazo
Mamlaka za Kyiv zimesema miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa ni mashariki mwa mkoa wa Kharkiv bambapo ghorofa inayotumika kama makazi ya watu iliangukiwa na kombora.
Miundombinu ya nishati na reli yalengwa
Akiyazungumzia mashambulizi hayo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameeleza kuwa mashambulizi hayo ya Urusi yalihusisha droni zipatazo 480 na makombora 29 yaliyolenga sekta ya nishati na miundombinu ya reli katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Sehemu ya bandari katika mkoa wa Odesa ililengwa pia hali iliyosababisha makontena yaliyokuwa na mafuta kushika moto na kuteketeza ghala la nafaka.