Migogoro
Mashambulizi ya droni yawauwa watu wawili Ukraine
18 Januari 2026
Matangazo
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema mashambulizi hayo yamehusisha zaidi ya droni 200. Zelensky kupitia ukurasa wake wa jukwaa la X ameongeza kuwa maeneo yaliyolengwa na Urusi ni pamoja na Kharkiv, Dnipro, Zaporizhzhia, Khmelnytskyi, na Odesa
Zaidi ya watu 200,000 hawana umeme Zaporizhzhia
Wakati huohuo Gavana wa eneo la Zaporizhzhia la Ukraine linalodhibitiwa na Urusi kwa aslilimia 75 Yevgeny Balitsky amesema zaidi ya watu 200,000 hawana umeme baada ya mashambulizi ya droni yaliyofanywa na Ukraine jana Jumamosi.