1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel Gaza yaua watu 8 wa familia moja

17 Desemba 2024

Shambulizi la Israel mjini Gaza limewaua watu wanane wa familia moja wengi wakiwa wanawake na watoto, hii ikiwa ni kulingana na maafisa wa afya wa Palestina.

Gazastreifen Khan Yunis | Tote bei Israelischem Angriff auf eine Schule
Wapalestina waliofurushwa makwao wakikagua uharibifu kufuatia mashambulizi la Israel huko Khan Yunis, Gaza Desemba 16, 202.Picha: Hani Alshaer/Anadolu/picture alliance

Shambulizi hilo lililofanyika siku ya Jumatatu usiku lililenga nyumba moja katikati mwa Gaza katika eneo jirani la Daraj. Miongoni mwa miili iliyopatikana na ya baba na wanawe watatu pamoja na bibi ya watoto hao. Israel bado haijatoa tamko lolote juu ya shambulizi hilo. Kulingana na wizara ya afaya ya Gaza, kwa ujumla mashambulizi ya Israel mjini humo yamesababisha mauaji ya watu zaidi ya 45,000 ndani ya miezi 14 na wengi wa waliouwawa ni wanawake na watoto. Israel ilianzisha awamu hii ya mashambulizi yake kwenye Ukanda wa Gaza kujibu mashambulizi ya kundi la Hamas kusini mwa Israel yaliyosababisha mauaji ya watu 1,200.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW