1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mashambulizi ya Israel yajeruhi 6 Syria

29 Aprili 2023

Raia watatu wa Syria wamejeruhiwa hii leo, kufuatia mashambulizi ya anga ya Israel karibu na mji wa Homs. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la nchini humo-SANA

Syrien | Jandaris Erdbeben
Picha: Mahmoud Hassano/REUTERS

Taarifa hiyo imesema pamoja na idadi hiyo ya majeruhi, kituo cha mafuta kimeungua moto na matanki kadhaa ya mafuta yameteketea. Imeeleza pia kuwa jeshi la Syria lilifanikiwa kidhibiti baadhi ya makombora.Hata hivyo jeshi la Israel halikuweza kusema chochote kufuatia tukio hilo ingawa Shirika la Uangalizi wa Haki za Binaadamu la Syria lenye maskani yake Uingereza lilisema  Israel iliharibu ghala la silaha la kundi la Hezbollah la nchini Lebanon, katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Dabaa kwenye maeneo ya vijijini ya mkoa wa HomsKatika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja cha vita nchini Syria, Israel imefanya mamia ya mashambulizi ya anga, yenye kuwalenga wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran na wapiganaji wa kundi la Hezbollah pamoja na maeneo ya jeshi la Syria.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW