1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yamuua afisa mawasiliano wa Hezbollah

18 Novemba 2024

Mashambulizi ya Israel yamesababisha hapo jana vifo vya makumi ya watu Gaza na Lebanon.

 Mohammed Afif ndiye aliyeuawa katika shambulio la Israel huko Beirut.
Afisa mawasiliano wa Hezbollah Mohammed Afif ndiye aliyeuawa katika shambulio la Israel huko Beirut. Picha: Houssam Shbaro/Anadolu/picture alliance

Katika Ukanda wa Gaza karibu watu 12 wameripotiwa kuuawa huku mashirika ya Umoja wa Mataifa yakitahadharisha kuhusu hali mbaya ya kibinaadamu.

Wizara ya afya huko Gaza inayodhitiwa na kundi la Hamas imesema idadi jumla ya vifo katika zaidi ya miezi 13 ya vita imefikia watu 43,846.

Huko nchini  Lebanon , mashambulizi ya Israel yameua watu 11 eneo la kusini na sita katika mji mkuu wa Beirut, akiwemo Afisa mawasiliano wa Hezbollah Mohammed Afif.

     

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW