1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yasababisha vifo vya watu 10

4 Novemba 2024

Mashambulizi ya anga ya Israel yamewaua Wapalestina 10 leo Jumatatu na kuwajeruhi wengine kadhaa kwenye Ukanda wa Gaza, hayo ikiwa ni kulingana na duru za kiafya na huduma za dharura kwenye eneo hilo.

Ukanda wa Gaza | Athari za mashambulizi ya Israel
Mwanamume akimuokoa mwanamke kutoka kwenye jengo lililoshambuliwa na vikosi vya Israel huko Gaza.Picha: Moiz Salhi/Anadolu/picture alliance

Taarifa zinasema 7 kati yao wameuwawa kwenye shambulizi lililozilenga nyumba mbili katika mji wa kaskazini mwa Gaza wa Beit Lahiya na wengine watatu wamepoteza maisha baada ya ndege za Israel kuishambulia kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Nuseirat. 

Wapalestina wanasema mashambulizi mapya ya anga na ardhini yanayofanywa na Israel yanalenga kuwalazimisha watu kuikimbia miji miwili ya kaskazini mwa Gaza ili kuacha kipande cha ardhi kitakachotumiwa na vikosi vya Israel. 

Soma pia:Mashambulizi ya Israel yawauwa watu 10 Gaza

Israel yenyewe inakanusha madai hayo ikisema kinachoendelea ni juhudi zake za kupambana na wapiganaji wa kundi la Hamas wanaofanya mashambulizi kutokea maeneo hayo. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW