MigogoroMashariki ya Kati
Mashambulizi ya Israel yauwa 10 Ukanda wa Gaza
5 Novemba 2024Matangazo
Haya yamesemwa na maafisa wa Palestina. Maafisa hao wanadai kwamba katika Ukingo wa Magharibi, vikosi vya Israel vimewauwa watu 2 kufuatia kombora la angani na mtu wa tatu akauwawa kwa kupigwa risasi.
Haya yanafanyika wakati ambapo waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken ametoa wito wa msaada zaidi kuwasilishwa katika Ukanda wa Gaza kutokana na hali mbaya ya kiutu inayoshuhudiwa katika eneo hilo, zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuanza kwa vita vya Israel dhidi ya wanamgambo wa Hamas.
Soma pia:Mashambulizi ya Israel yawauwa watu 10 Gaza
Taarifa ya wizara ya ulinzi ya Marekani iliyotolewa na msemaji wa wizara hiyo Mathew Miller imesema kwamba Blinken alijadiliana na Miller kwa njia ya simu kuhusiana na hali ya kiutu huko Gaza.