1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yauwa 7 Lebanon

9 Novemba 2024

Wizara ya afya ya Lebanon, imesema watu saba, wakiwemo watoto wawili, wameuwawa katika shambulizi la Israel katika mji wa kusini wa Tyre.

Israel, Lebanon, Tyre
Majengo yaliyoporomoshwa na mashambulizi ya anga ya Israel katika mji ya Tyre nchini Lebanon.Picha: Kawnat Haju/AFP

Kundi la waokoaji liliendelea kutafuta miili kadhaa chini ya vifusi vya majengo yaliyoharibiwa na hivyo idadi kamili ya waliouawa huenda ingeliongezeka.

Watu wengine 46 walijeruhiwa katika shambulizi hilo.

Wizara hiyo pia ilisema sehemu ya miili iliyopatikana itatambuliwa kwa kutumia vipimo vya vinasaba.

Soma zaidi: Israel yaendeleza mashambulizi yake Gaza na Lebanon

Picha za shirika la habari la AFP zilionesha waokoaji wakibeba miili kutoka kwenye vifusi vya majengo yaliyoharibiwa vibaya. 

Vita kati ya Hezbollah na Israel vilipamba moto baada ya kundi hilo kuanza kuishambulia Israel kufuatia mashambulizi yake inayofanya kwa watu wa Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW