1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wizara ya Afya Gaza: Mashambulizi ya Israel yauwa 70

25 Desemba 2023

Mashambulizi yaliyofanywa na Israel jana katika kambi ya wakimbizi ya Al-Maghazi huko Ukanda wa Gaza, yamesababisha vifo vya takriban watu 70, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza.

Gaza | Mzozo wa Mashariki ya Kati | Mapambano
Vita vya Gaza vimesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 20,000.Picha: Menahem Kahana/AFP

Msemaji wa wizara hiyo, amesema familia kadhaa katika eneo la Al-Maghazi ziliathiriwa na mashambulizi hayo.

Shirika la habari la Ujerumani, DPA, halikuweza kuthibitisha taarifa hizo kwa uhuru. Msemaji wa jeshi la Israeli amesema ripoti hizo zinachunguzwa.

Wanajeshi wa Israel wamekuwa wakifanya mashambulizi katika Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7, baada ya kundi la wanamgambo la Hamas na makundi mengine yenye itikadi kali ya Palestina, kufanya mashambulizi dhidi ya Israel, ambapo takriban watu 1,200 waliuawa na zaidi ya 240 kushikwa mateka.

Israel, Marekani na Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa nchi ambazo zimeliorodhesha Hamas kuwa kundi la kigaidi.

Kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza, zaidi ya watu 20,258 wameshauawa katika Ukanda huo tangu mwanzo wa vita hivyo na 53,688 wamejeruhiwa, hasa raia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW