1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Mashambulizi ya Israel yawaua Wapalestina 11, Gaza City

17 Oktoba 2024

Mashambulizi ya Israel yamewauwa Wapalestina 11 huko Gaza siku ya Allhamisi. Haya ni kwa mujibu wa madaktari katika eneo hilo.

Gaza I Mashambulizi yaripotiwa Gaza City
Maafa zaidi yaendelea kushuhudiwa kufuatia kutanuka kwa mzozo wa Mashariki ya katiPicha: Abdel Kareem Hana/AP/picture alliance /

Haya yanafanyika wakati ambapo jeshi la Israel limepeleka magari ya kivita katika eneo la kaskazini la Jabalia ambako Wapalestina na maafisa wa Umoja wa Mataifa wametahadharisha kuhusu ukosefu wa chakula na madawa.

Raia wa Jabalia wamesema jeshi la Israel limelipua nyumba kadhaa kwa mashambulizi ya angani, mizinga na kutega mabomu katika majengo.

Huduma ya dharura ya Gaza imesema imewaokoa watu kadhaa waliojeruhiwa waliokuwa wamejificha katika shule moja iliyoshika moto baada ya kushambuliwa na kombora la Israel.

Jeshi la Israel kwa upande wake limesema limeyakubalia malori 50 ya msaada wa kiutu kuingia kaskazini mwa Gaza.

Wakati huo huo, jeshi la Syria linasema Israel imewajeruhi raia wawili na kuharibu kambi ya kijeshi mapema leo katika shambulizi lililofanywa kwenye mji wa pwani wa Latakia nchini humo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW