1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yawaua watu 30 Gaza

3 Januari 2025

Watu wapatao 30 wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel katika Ukanda wa Gaza, tangu Ijumaa asubuhi.

Shirika la habari la Kipalestina WAFA, limeripoti kuwa miongoni mwa waliouawa ni mwandishi habari
Shirika la habari la Kipalestina WAFA, limeripoti kuwa miongoni mwa waliouawa ni mwandishi habariPicha: Mohammed Alaswad/AP

Jeshi la Israel halijazungumzia mashambulizi hayo. Hata hivyo, limeeleza kuwa jana iliyalenga kwa mashambulizi ya anga, maeneo 40 ya wapiganaji wa Hamas katika Ukanda wa Gaza. Taarifa ya jeshi hilo imeeleza kuwa baadhi ya maeneo yalikuwemo ndani ya majengo ya shule.

Wakati huo huo, jeshi la Israel limesema makombora mawili yamerushwa kutokea kaskazini mwa Gaza leo, ikiwa ni mfululizo wa mashambulizi ya hivi karibuni yanayofanywa kutoka katika ardhi ya Palestina.

Kombora moja limeangukia karibu na eneo la Nir Am, na jengine liliangukia kwenye eneo la wazi. Hakuna madhara yoyote yaliyoripotiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW