1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mashambulizi ya Israel yawaua watu 40 Gaza

15 Oktoba 2024

Mashambulizi ya jeshi la Israel yameuwa Wapalestina takribani 40 katika Ukanda wa Gaza.

Gaza I Mashambulizi ya Israel kwenye eneo la mahema huko Deir al Balah
Gaza I Mashambulizi ya Israel kwenye eneo la mahema huko Deir al BalahPicha: Abdel Kareem Hana/AP/picture alliance

Maafisa wa afya wa Palestina wamesema takribani watu 11 waliuawa karibu na Al-Falouja karibu na Jabalia, huku wengine 10 wakiuawa Bani Suhaila, mashariki mwa Khan Younis. 

Mapema leo, shambulizi la anga la Israel liliharibu nyumba tatu huko Sabra, na miili miwili iligunduliwa katika eneo hilo, huku zoezi la kuwatafuta watu wengine 12 wanaoaminika kuwemo ndani ya nyumba hizo likiendelea. 

Soma pia:Mashambulizi ya Israel huko Gaza yaua watu 8 wa familia moja 

Watu wengine watano waliuawa wakati nyumba yao iliposhambuliwa katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, katikati ya Gaza. 

Ofisi ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa imesema leo kuwa jeshi la Israel linaonekana kulitenganisha kabisa eneo la kaskazini ya Gaza na Ukanda wa Gaza. 

Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umesema watoto 400,000 nchini Lebanon wamekosa makaazi katika vita vya wiki tatu.