1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yawauwa 22 Beirut

11 Oktoba 2024

Mashambulizi ya Israel katika eneo la katikati mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut yamewauwa watu 22, wengine chungunzima wakajeruhiwa na kusababisha uharibifu mkubwa.

Libanon Shebaa | Israelischer Drohnenangriff | Friedenssoldaten der UNIFIL verletzt
Picha: Stringer/dpa/picture alliance

Mashambulizi hayo ya anga yameporomosha jengo moja la ghorofa nane na jingine kuharibiwa vibaya. Jeshi la Israel limesema litachunguza kuhusu mashambulio hayo.

Kituo cha Televisheni kinachoendeshwa na kundi la Hezbollah, cha Al Manar kimeripoti kwamba jaribio la kumuua afisa mwandamizi wa shughuli za usalama wa kundi hilo Wafiq Wafa halikufanikiwa.

Kituo hicho kimesema Wafa hakuwemo kwenye majengo yaliyoshambuliwa na Israel.

Mashambulio ya Israel dhidi ya maeneo yanayokaliwa na wakaazi kusini mwa mji mkuu Beirut yameongezeka.

Kundi la Hezbollah linaendesha operesheni zake nyingine kwenye eneo hilo la Kusini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW