1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yawauwa Wapalestina 17 Gaza

Angela Mdungu
10 Novemba 2024

Watu wasiopungua 17 wameuwawa kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel ya Jumapili yaliyolenga jengo lililokuwa likiwahifadhi watu wasio na makazi katika Ukanda wa Gaza.

Vita Ukanda wa Gaza
Sehemu ya Gaza inavyoonekana baada ya mashambulizi ya anga ya IsraelPicha: Bashar Taleb/AFP

Kulingana na Mkurugenzi wa hospitali ya Al Ahly katika mji wa Gaza Daktari Fadel Naim, waliouwawa ni pamoja na wanawake tisa na huenda idadi ikaongezeka.

Soma zaidi: Wapalestina 43,508 wauawa Gaza

Amesema watu hao wameuwawa katika nyumba hiyo kwenye kambi ya Jabaliya ambako Israel imekuwa ikifanya mashambulizi kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa. Jeshi hilo limeizingira Jabaliya na miji jirani ya Beit Lahiya na Beit Honoun kwa miezi kadhaa na kuruhusu kiasi kidogo cha misaada ya kiutu kufikia maeneo hayo. Maelfu ya watu wamekimbilia katika maeneo jirani.

Kwa upande mwingine Qatar imejiondowa kwenye nafasi yake ya kuwa mpatanishi mkuu katika kutafuta makubaliano ya kusitisha mapigano ya Gaza na kuachiliwa kwa mateka.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW