1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yawauwa watu 12 Gaza

18 Desemba 2024

Shirika la ulinzi wa raia la Gaza limesema takriban watu 12 wameuawa na mashambulizi ya anga ya Israel, wengi wao wakiwa wakimbizi waliokuwa wametafuta hifadhi katika nyumba moja kaskazini mwa ukanda wa Gaza.

Gazastreifen Khan Yunis | Tote bei Israelischem Angriff auf eine Schule
Picha: Hani Alshaer/Anadolu/picture alliance

Msemaji wa shirika hilo Mahmud Bassal ameliambia shirika la habari la AFP kuwa Wapalestina 10 wameuawa kufuatia shambulio la Israel lililolenga nyumba moja katika eneo la Beit Lahia.

Bassal ameongeza kuwa mtoto mmoja ameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio lingine tofauti lililolenga nyumba karibu na eneo la Jabalia, sehemu ambayo vikosi vya Israel vimeelekeza oparesheni zao katika miezi ya hivi karibuni.

Zaidi ya miezi 14 tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas, Marekani imeeleza matumaini kuhusu uwezekano wa kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano ukanda wa Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW