1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya mtandaoni yatibuwa dunia

13 Mei 2017

Wimbi la mashambulizi ya mtandao Ijumaa (12.05.2017) limepiga kwa haraka duniani kwa kutumia kile kinachoonekana kama kasoro iliosababishwa na kuvuja kwa nyaraka kutoka kwa Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani.

Symbolbild Hackerangriff
Picha: picture alliance/dpa

Mashambulizi hayo ambayo wataalamu wanasema yameziathiri takriban nchi kadhaa duniani yametumia mbinu inayojulikana kama "ransomware"ambayo hutishia kuyafunga majalada binafsi ya watumiaji venginevyio wanalipa washambuliaji kima fulani cha sarafu ya Uingereza inyotumika kwenye digitali.

Miongoni mwa waathirika wa shambulio hilo ni mitandao ya kompyuta katika hospitali nchini Uingereza,wizara ya mambo ya ndabi ya Urusi ,kampuni kubwa kabisa ya mawasiliano ya simu ya Uhispania na kampuni ya kusafirisha vifurushi ya Marekani FedEx na mashirika mengine mengi.

Kituo cha Taifa cha Usalama wa Mtandao nchini Uingereza na Shirika lake la Taifa la Uhalifu zimekuwa zikichunguza visa hiyvo kwa upande wa Uingereza ambapo vimetimuwa huduma katika vituo vya kutowa huduma za afya vya taifa.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema shambulio hili halikulenga tu vituo vya huduma za afya vya taifa nchini Uingereza NHS bali ni shambulio la kimataifa na nchi na mashirika kadhaa yameathirika.

Serikali ya Uingereza haijuwi bado nani amehusika na shambulio hilo la mtandao duniani hapo Ijumaa ambalo limetibuwa mfumo wa afya nchini Uingereza.

Haijulikani nani mhusika

Kituo cha Taifa cha Usalama wa Mtandao nchini Uingereza.Picha: picture-alliance/PA Wire/D. Lipinski

Waziri wa mambo ya ndani Amber Ruud ameiambia radio ya BBC hapo Jumamosi kwamba "hatuwezi kusema nani amehusika na shambulio hilo na kwamba kazi bado inaendelea."

Amesema Kituo cha Taifa cha Usalama wa Mtandao kimekuwa kikishirikiana na shirika la huduma za afya la taifa nchini humo kuhakikisha shambulio hilo linadhibitiwa na haliwi kubwa wakati Shirika la Uhalifu la Taifa linashirikiana nao kujuwa limetokea wapi.Rudd amesema serikali haijuwi iwapo shambulio hilo limeongozwa na serikali ya kigeni.

Wizara ya mambo ya mambo ya ndani ya Urusi imesema baadhi ya kompyuta zake zimekumbwa na "shambulio hilo la virusi" na kwamba juhudi zinafanyika kuvitomokeza virusi hivyo.

Timu ya kukabiliana na hali ya dharura ya wizara ya ulinzi wa dani nchini Marekani imesema inatambuwa maambukizi hayo ya virusi vya kutishia kufuta majalada ya watu binafsi na kudai fedha za ugombozi ili isichukuwe hatua hiyo yako katika nchi kadhaa duniani.

Nchi 99 zaathirika

Gari la kubebea wagonjwa likisubiri katika Hospitali ya St.Thomas London,Uingereza.Picha: Reuters/S. Wermuth

Jakub Kroustek wa kampuni ya usalama ya Avast amesema katika maandishi yaliyowekwa kwenye blogu "Hivi sasa tunaona kugundilika kwa mashambulizi zaidi ya 75,000 katika nchi 99.

Mtafiti wa kampuni ya Kaspersky Costin Raiu ametaja mashambulizi 45,000 katika nchi 74 akisema kirusi hicho kinachotishia kufuta majalada na kudai fedha kinachojibadilisha wenyewe kimekuwa kikienea kwa haraka.

Katika maabara ya Kaspersky imesema katika imekuwa ikijaribu kuyakinisha iwapo inawezekana kusoma mafumbo ya data zilizofungwa katika shambulio hilo kwa lengo la kuwa na zana za kutowa ufafanuzi haraka iwezekanavyo.

Maabara ya kampuni ya usalama ya Forcepoint nayo imesema katika taarifa kwamba shambulio hilo lina taathira kwa dunia na limeathiri mitandao nchini Australia,Ubelgiji,Ufransa,Ujerumani,Italia na Mexico.

Kirusi chatowa tishio na kudai fedha

Shirika la Reli la Ujerumani Deutsche Bahn miongoni mwa waathirika.Picha: picture-alliance/dpa/J. Woitas

Nchini Marekani kampuni ya FedEx  imekiri kwamba imekumbwa na kirusi hicho chenye kutishia kufuta majalada na kudai fedha na kwamba imekuwa ikitekeleza hatua za marekebisho haraka iwezekanavyo.

Shirika la Huduma za Afya la Taifa nchini Uingereza limetangaza kutokea kwa kisa kikubwa kufuatia shambulio hilo ambalo limelilazimisha baadhi ya hospitali kugeuza safari za magari ya kubebea wagonjwa na kufuta operesheni.

Kopmyuta za kampuni ya Reli ya Ujrumani Deutche Bahn pia zimeathirika ambapo kampuni hiyo imeripoti Jumamosi asuhubuhi kwamba mabango ya elektroniki ya kuonyesha matagazo katika vituo vya benkin hiyo yameathirika.

Mashambulizi hayo ya mtandaoni yanatilia mkazo ukweli juu ya uwerekano huo wa kuathirika kwa urahisi kunaweza kutumiwa vibaya na sio tu mashirika ya kijasusi bali pia na wadukuzi na wahalifu duniani kote.

Mwandishi : Mohamed Dahman/AFP/Reuters

Mhariri : Zainab Aziz