1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIraq

Iraq: Roketi zafyetuliwa kuelekea kambi ya jeshi la Marekani

26 Julai 2024

Maafisa wa usalama wamesema roketi kadhaa zimefyetuliwa kuelekea kambi ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani nchini Iraq.

Wanajeshi wa Marekani wakati wa hafla ya kukabidhi kambi ya kijeshi ya Taji kutoka kwa wanajeshi wa muungano unaoongozwa na Marekani kwa vikosi vya usalama vya Iraq.
Wanajeshi wa Marekani wakati wa hafla ya kukabidhi kambi ya kijeshi ya Taji kutoka kwa wanajeshi wa muungano unaoongozwa na Marekani kwa vikosi vya usalama vya Iraq. Picha: Thaier Al-Sudani/File PhotoU*/REUTERS

Duru za usalama za Iraq zimeeleza kuwa roketi nne zimeanguka karibu na kambi ya jeshi ya Ain al-Assad iliyoko mkoa wa Anbar.

Afisa wa Marekani amesema ripoti za awali zimeonyesha kuwa mashambulizi hayo ya roketi yalilenga nje ya kambi walimokuwa japo hayakusababisha majeruhi au uharibifu. Hata hivyo, hakuna kundi lolote lililojitokeza kudai kuhusika na hujuma hiyo.

Soma pia: Mripuko wauwa mmoja, wajeruhi wanane Iraq

Mashambulizi hayo yametokea baada ya kufanyika mkutano wa kiusalama wiki hii kati ya maafisa wa Iraq na Marekani mjini Washington kuhusu mustakabali wa muungano huo wa kijeshi unaoongozwa na Marekani nchini Iraq.

Makundi yanayoungwa mkono na Iran yamekuwa yakiushinikiza muungano huo uondoke nchini humo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW