1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mashambulizi ya Ukraine yaua watu 28, Kherson na Luhansk

Sylvia Mwehozi
8 Juni 2024

Mashambulizi ya Ukraine katika mikoa inayokaliwa na Urusi ya Kherson na Luhansk, yamesababisha vifo vya takribani watu 28 kwa mujibu wa maafisa wa mikoa hiyo wanaoungwa mkono na Moscow.

Ukraine-vita- droni
Ndege ya droni ya Urusi Picha: Andrei Rubtsov/Tass/dpa/picture alliance

Mashambulizi ya Ukraine katika mikoa inayokaliwa na Urusi ya Kherson na Luhansk, yamesababisha vifo vya takribani watu 28 kwa mujibu wa maafisa wa mikoa hiyo wanaoungwa mkono na Moscow.

Gavana wa mkoa wa Kherson Vladimir Saldo amenukuliwa na Shirika la habari la Urusi, TASS, akisema kuwa vikosi vya Ukraine, kwanza vilishambulia mji huo kwa bomu lililotengenezwa na Ufaransa, kisha kushambulia tena kwa kombora la HIMARS lililotolewa na Marekani.Ukraine yaamuru watu kuhamishwa maeneo ya mkoa wa Donetsk

Ukraine na Urusi zote zimeendelea kushambuliana kwa droni katika mashambulizi ya usiku kucha.Droni zipatazo 25 za Ukraine zimeripotiwa kudunguliwa katika mikoa ya kusini mwa Urusi ya Kuban na Astrakhan, mkoa wa magharibi wa Tula na Rasi ya Crimea.

Ukraine pia imedai kudungua Droni 9 kati ya 13 za Urusi katika mikoa yake ya Poltava, Zaporizhzhia, Dnipropetrovsk na Kharkiv.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW