1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine yawaua watu kadhaa

18 Novemba 2024

Mashambulizi makali ya makombora na droni ya Urusi dhidi ya Ukraine ya kuanzia jana Jumapili yamesababisha vifo vya watu kadhaa na kuwajeruhi wengi.

Ukraine | Urusi yaushambulia mji wa Sumy
Mwanajeshi wa kikosi cha zimamoto akizima moto katika jengo la makazi lililoshambuliwa na Urusi katika mji wa Sumy nchini Ukraine, Novemba 17, 2024 Picha: State Emergency Service of Ukraine in Sumy region/Handout/REUTERS

Kaimu meya wa mji wa Sumy ulioko kaskazini mashariki mwa Ukraine, alisema usiku wa kuamkia leo Jumatatu kwamba watu wasiopungua 10 waliuawa na zaidi ya 50 wamejeruhiwa.

Mashambulizi hayo yaliyolenga pakubwa miundombinu ya nishati, yamesababisha umeme kukatika katika maeneo mengi ya Ukraine, ikiwemo mji mku Kiev, Odessa na Sumy.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kupitia ukurasa wake wa Telegram kwamba, mifumo ya ulinzi ya angani ya Ukraine iliharibu makombora 120 na droni 90 zilifyatuliwa na Urusi.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema vita vinavyoendelea vya Urusi dhidi ya Ukraine ni sawa na uhalifu wa kivita.