1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yauwa katika mashambulizi Zaporizhzhia

8 Aprili 2024

Watu watatu wameuawa baada ya Urusi kulishambulia jimbo la kusini mwa Ukraine la Zaporizhzhia mapema hii leo, katika siku ya pili ya mashambulizi makubwa katika eneo hilo.

Ukraine Saporischschja  Raketenangriffe Ruinen
Picha: REUTERS

Gavana wa jimbo hilo Ivan Federov amesema kupitia mitandao ya kijamii kwamba watu wengine watatu wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo, siku moja baada ya watu watatu kuuawa katika shambulizi lililofanywa kwenye mji wa Gulyaipole.

Jeshi la anga la Ukraine aidha limesema Urusi imeanzisha mashambulizi mapya ya droni ikiilenga miundombinu muhimu, ambayo ni pamoja na kituo cha mafuta, amesema gavana wa odesa, Oleh Kiper.

Shambulizi hili linafanywa siku moja baada ya kinu cha Nyuklia cha Zaporizhzhia kushambuliwa na droni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW