1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Urusi Ukraine yaharibu miundombinu

17 Novemba 2025

Shirika la huduma za dharura Ukraine limesema mashambulizi ya Urusi kusini mwa mji wa Odesa, yamesababisha moto mkubwa katika miundombinu ya nishati na bandari.

Vita vya Urusi na Ukraine
Shambulizi la Urusi Mashariki mwa mji wa Kharkiv limesababisha mauaji ya watu watatu na kuwajeruhi wengine zaidi ya 10 Picha: Oleskandr Kornyakov

Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Oleksii Kuleba amesema shambulizi hilo linasemekana kuharibu maeneo makubwa ya bandari na meli kadhaa za raia zilizokuwa karibu.

Kuleba amesema umeme umekatika katika sehemu moja ya bandari, lakini tayari wataalamu wanashughulikia tatizo hilo ili kurejesha huduma hiyo muhimu haraka iwezekanavyo.

Kwengineko shambulizi jengine la Urusi Mashariki mwa mji wa Kharkiv limesababisha mauaji ya watu watatu na kuwajeruhi wengine zaidi ya 10 hii ikiwa ni kulingana na msimamizi wa jeshi wa eneo hiloVitaliy Karabanov.

Idadi ya waliouwawa huenda ikapanda kutokana na utawala nchini humo kuendelea kupokea taarifa za athari za shamnbulizi hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW