Mashambulizi ya Urusi Ukraine yawajeruhi sita mjini Odesa
31 Desemba 2025
Kiongozi wa Jeshi mjini humo Oleg Kiper, amesema mashambulizi hayo ya droni yalivurumishwa kuilenga miundumbionu ya nishati, na makaazi ya watu.
Taarifa zaidi zinasema mwanamume wa miaka 42 pia alijeruhiwa na yuko katika hali mbaya hospitalini. Kwa sasa sehemu ya mji huo haina umeme pamoja na maji. Kwengineko mashambulizi mengine ya droni kutoka Urusi yaliwajeruhiu watu wawili katika jimbo la Dnipropetrovsk.
Mashambulizi haya yanajiri baada ya Ukraine kukanusha kushambulia makazi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na kuituhumu Moscow kusema uwongo ili kusambaratisha mazungumzo ya kusitisha vita Ukraine. Moscow imesema kitendo ilichofanyiwa nchi yake ni cha kigaidi.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, aliyesema madai ya Urusi ni ya kupanga, atakutana na washirika wake Januari 6 nchini Ufaransa katika juhudi za kuendeleza juhudi za kusaka amani.