Mashambulizi ya Urusi yamuuwa baba na wanawe watatu
11 Februari 2026
Matangazo
Haya yamesemwa leo na maafisa wa Ukraine.
Afisi ya mwendesha mashtaka wa eneo la Kharkiv amesema droni hiyo imeishambulia nyumba moja iliyokuwa makao ya watu watano na 4 kati yao baba na wanawe watatu wakaaga dunia, huku mama yao ambaye ni mjamzito akiokolewa.
Kulingana na jeshi la anga la Ukraine, Urusi imeishambulia Ukraine na droni 129 usiku kucha, huku droni 112 kati ya hizo zikidunguliwa.
Kharkiv ambalo ni eneo lililo kilomita 30 kutoka mpaka wa kaskazini mashariki wa nchi hiyo limekuwa eneo ambalo limelengwa mara kwa mara na mashambulizi ya angani ya Urusi.