Mashambulizi ya Urusi yasababisha maafa Ukraine
24 Januari 2026
Maafa hayo yametokea katika wakati ambapo wajumbe wanaoshiriki mazungumzo ya amani kutoka Ukraine, Urusi na Marekani wakitarajiwa kukutana Abu Dhabi leo kwa siku ya pili ya mazungumzo ya kumaliza uvamizi huo wa Urusi wa takriban miaka minne.
Kulingana na kiongozi wa jeshi mjini Kyiv Tymur Tkachenko, mtu huyo mmoja aliuawa na wengine wanne wamejeruhiwa katika shambulizi la droni la Urusi kwenye mji mkuu Kyiv.
Wengine 19 wamejeruhiwa kwenye mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine wa Kharkiv. Hayo yameelezwa na Meya wa mji huo Ihor Terekhov.
Mazungumzo ya wajumbe hao wa mataifa hayo matatu, ni tukio la kwanza linalojulikana ambapo maafisa wa utawala wa Marekani wamekaa na nchi zote mbili Ukraine na Urusi kama sehemu ya msukumo wa Washington wa kutaka kumaliza uvamizi huo wa Urusi nchini Ukraine.