1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Urusi yaua sita Ukraine

1 Oktoba 2024

Urusi imefanya mashambulizi yaliyoolilenga soko moja la mji wa kusini mwa Ukraine wa Kherson na kuuwa watu sita na kuwajeruhi wengine watatu.

Ukraine, Kherson, Urusi
Athari ya mashambulizi ya Urusi kwenye mji wa Kherson kusini mwa Ukraine.Picha: picture alliance/Anadolu

Kwa mujibu wa maafisa wa Ukraine, mashambulizi hayo yalifanyika asubuhi ya Jumanne (Oktoba 1), wakati raia kote nchini humo walikuwa wakitowa heshima zao kwa wanajeshi na watu waliouwawa kwenye vita vinavyoendelea kwa kukaa kimya kwa dakika moja.

Soma zaidi: Watu saba wauawa kwa shambulizi la Urusi nchini Ukraine

Gavana wa eneo hilo, Oleksandar Prokudin, alichapisha video iliyoonesha miili ya watu waliouwawa ikiwa imelala karibu na maduka ikiwa imefunikwa na nyanya na mboga mboga.

Taarifa pia zinasema Urusi iliwakamata watu kiasi 39 iliyowaita wafuasi wa makundi ya kigaidi ya Ukraine.